Connect with us

Soka

Yanga Yatinga Nusu Fainali

Klabu ya Yanga sc  imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuifunga timu ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kagera walikua wa kwanza kupata bao dakika ya 19 kupitia kwa Awesu Awesu huku Yanga wakisawazisha dakika ya 51 kupitia kwa David Molinga na dakika ya 71 Mrisho Ngassa alifanyiwa madhambi nje kidogo ya mstari wa 18 lakini mwamuzi aliamuru iwe penati na Deus Kaseke akaifungia goli la pili.

Awese Awese alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Kagera kumaliza mchezo wakiwa pungufu japo walimiliki mchezo mpaka filimbi ya Mwisho.

Yanga itawalazimu kusubiri mpambano kati ya Simba sc dhidi ya Azam fc ili kujua watakayekutana nae kuelekea hatua ya fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka