Connect with us

Soka

Yanga yaitandika Biashara Utd

Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga imepata ushindi wa 2-1 dhidi Biashara united kwenye moja ya mechi ngumu iliyokutana nazo msimu huu kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa muda mchache uliopita.

Biashara waliishangaza Yanga mapema tu kwa kupata bao dakika ya 2 tu ya mchezo kupitia kwa Atupele Green baada ya utumia vema makosa ya mlinda mlango Djigui Diarra aliyeshindwa kudaka vizuri mpira.

Wananchi walirejea mchezoni kwa kasi wakitaka kusawazisha bao hilo,lakini kukosekana kwa utulivu kuliwafanya washindwe kutengeneza nafasi za kutosha.Uwezo binafsi wa mshambuliaji Fiston Mayele uliwawezesha kwenda mapumziko wakiwa 1-1 baada ya kupiga akrobati iliyozaa basi dakika ya 42.Dakika ya 79 Saido Ntibanzonkiza aliiandikia timu hiyo bao la pili kwa mkwaju wa penati.

Licha ya kwenda kwenye mchezo huo bila ya kocha wake mkuu Mkenya Odhiambo,lakini wanajeshi hao wa mpakani walikuja Dar es salaam kupata pointi,hii ni kutokana na na kufanya mashambulizi mengi ya kushtukiza na kama wangekuwa makini basi wangeondoka na alama zote tatu.Mlinda mlando wa Yanga Diarra aliokoa mipira miwili ya hatari ambayo huenda ingebadilisha matokeo ya mchezo kama ingetinga wavuni.

Yanga imeendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya mechi za mzunguko wa kumi wakiwa na alama 26 mbili mbele ya watani wao wa jadi Simba.Mchezo ujao wa ligi wananchi watacheza na watoza ushuru Dodoma Jiji katika dimba la Mkapa kabla ya kwenda kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka