Connect with us

Soka

Yanga Watua TPLB

Uongozi wa klabu ya Yanga umepeleka malalamiko Bodi ya ligi (TPLB) juu ya faini walizopewa katika mechi zao zilizochezwa mwezi uliopita kutokana na kutoridhishwa na jinsi hatua hizo zilivyo chukuliwa dhidi yao.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli amesema kuhusu kupigwa faini ya shilingi laki tano kutokana na kuto wasilisha majina ya wachezaji katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons msemaji huyo amebainisha kuwa walipeleka kwa kuchelewa kwakua mechi ilihamishwa ghafla kutoka uwanja Sokoine kwenda Samora, Iringa baada ya kutokuwa tayari kuchezewa baada ya mvua kunyesha.

Kuhusu faini ya shilingi laki mbili kwa kutoingia kwenye vyumba rasmi katika mchezo dhidi ya Simba msemaji huyo alisema walipeleka malalamiko Bodi ya ligi kuwa vyumba vyao havikuwa salama na wakaruhusiwa kuingia katika vyumba vya timu B lakini wameshangaa kuona wamepigwa faini hiyo.

Pia kuhusu mashabiki wao kurusha chupa za maji katika mchezo huo ni kutokana na wao kupeleka malalamiko Bodi ya juu ya mambo mbalimbali ambayo wanaona wanaonewa.

Bumbuli ameongeza kuwa wanashangaa Bodi hiyo kuzuia pesa kutoka kwa mdhamini Vodacom bila kufanya majadiliano na klabu hiyo kitu ambacho ni kinyume na kanuni ambazo wameziweka wenyewe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka