Soka
YANGA, SIMBA ZAMSHINDWA STRAIKA MRWANDA
WAKATI Simba na Yanga zikipambana kupata saini ya mshambuliaji Mnyarwanda, Jacques Tuyisenge, klabu ya Petro Atletico ya Angola imeweka mzigo mezani wa kiasi cha Sh.Mil.335.
Kwa sasa nyota huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu za mataifa tofauti zikiwemo zile za Simba na Yanga ambazo nazo zimekuwa zikimuwania tangu msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Tuyisenge ambaye hucheza pacha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere katika kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ anataka mshahara wa Sh. Mil 18.
Meneja wa straika huyo, Patrick Gakumba ameliambia Spoti Xtra, kuwa kwa sasa Tuyisenge anaweza asitue katika klabu hizo kutokana na bei yake kuwa juu lakini Waangola hawamkosi. “Hakuna sehemu ambayo Tuyisenge amesaini hadi sasa.
Siyo huko Angola wala timu yoyote ile ambayo imekuwa ikihusishwa kumtaka, Jacques ni bado yupo Gor Mahia na anaendelea kuwepo huko na hapo Tanzania sidhani kama anaweza kuja.
“Mimi ninaendelea kusema kwamba kwa klabu yoyote ile ambayo inamtaka yeye Tuyisenge basi ..