Connect with us

Soka

Yanga Mpya Full Fiziki,Stamina na Pumzi

Baada ya kutumia takribani wiki moja na ushee katika kambi ya mazoezi katika chuo cha Biblia mkoani Morogoro chini ya kocha wa viungo Noel Mwandila sasa kikosi hicho kimeiva kwa kuwa na fiziki,stamina na nguvu za kutosha.

Katika mechi ya kirafiki dhidi ya akademi ya Tanzanite iliyopigwa mabao 10 huku staa Mrisho Ngasa akifunga mabao matatu kazi kubwa ilikua na kushambulia,kukaba na kumiliki mpira kwa pamoja na hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mazoezi hayo ya Mwandila.

Katika mazoezi hayo wachezaji wa kigeni wameonekana kuwa sawa hasa katika kasi na nguvu hali iliyomfurahisha kocha huyo aliyekuja Yanga akiwa na Mzambia mwenzake George Lwandamina ambaye aliikacha timu hiyo na kurejea Zesco Fc ya nchini kwao.

Hii ni mara ya pili kwa timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi kuu mara 27 kuweka kambi mkoani humo katika chuo cha bibilia kilichopo Bigwa mkoani Morogoro.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka