Connect with us

Soka

Yanga kubwa kuliko 1.5bn

Klabu ya Yanga inatarajiwa kumalizia kampeni yake ya kuichangia klabu hiyo iliyobatizwa “Kubwa kuliko” itakayofanyika 15 june katika ukumbi wa Diamond jubilee hall jijini Dar es salaam ambapo lengo kubwa la kampeni hiyo ni kupata kiasi cha shilingi bilioni 1.5.

Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi jijini Dodoma na kufanyika mikoa mbalimbali ina lengo la kukusanya kiasi cha shilingi 1.5 bilioni zitakazo tumika kwa usajili na matumizi mengine ya klabu msimu ujao.

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya maandalizi Ruhago David amesema maandalizi yametimia kwa asilimia 90 na lengo ni kukusanya kiasi hicho cha fedha ili kundeshea klabu msimu ujao.

Kuhusu viingilio vya tamasha hilo meza za bei ya juu zitauzwa kwa shilingi milioni 10 huku kiasi cha chini ni shilingi laki moja kwa mtu mmoja.

Wanachama na wapenzi wa Yanga wamekua na kawaida ya kuichangia timu yao baada ya kutokua na mfadhili tangu Yussuph Manji ajitoe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka