Connect with us

Soka

Wolves yaiadhibu Man Utd Old Trafford

Wolverhampton Wonderers wamepunguza kasi ya Manchester United katika kupigania nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kuwatandika 1-0 katika dimba la Old Trafford.

Bao pekee la mchezo huo liliwekwa kimiani na kiungo wa Kimataifa wa Ureno Joao Moutinho kunako dakika ya 82 kwa shuti kali nje ya kumi na nane.

Kocha wa Man Utd Ralf Rangnick aliendelea namkutumia na mfumo wa 4-2-2-2 huku akimkosa nahodha wake Harry Maguire kutokana na kuwa na adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kukusanya kadi tano za njano.

Wolves waliutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa wakifanikiwa kufanya majaribio ya kufunga zaidi ya 20 huku wakikosa mabao mengine ya wazi,kama sio uimara wa mlinda mlango David De Gea basi huenda wangeondoka na ushindi mnono zaidi.

Manchester United wamesahuka hadi nafasi ya saba baada ya michezo 19 na alama 31,akiwa nje ya nafasi nne za juu kwa alama tano japo ana mchezo mmoja mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka