Connect with us

Soka

Wenger Aula Fifa

Kocha wa zamani wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa maendeleo ya soka duniani na shirikisho la mpira duniani(Fifa) na kumaliza tetesi zilizoenea kuwa atajiunga na klabu ya Bayern Munchen ya Ujerumani.

Kocha huyo aliyeifundisha Arsenal kwa miaka 22 na kuisaidia kuchukua ubingwa na ligi mara tatu ameteuliwa baada ya kukaa bila kujihusisha moja kwa moja na mpira tangu aondoke klabuni hapo mwezi may mwaka jana.

“Naangalia mbele zaidi kuchukua changamoto hii muhimu duniani” alisema kocha wakati akihojiwa na shirika la habari la Bbc.

Kocha huyo baada ya kuchukua nafasi hiyo atajihusisha zaidi na maendeleo ya mpira kwa wanaume na wanawake pamoja na masuala ya kiufundi duniani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka