Connect with us

Soka

Wanajeshi Wampasua Kichwa Zahera

Kocha wa Yanga sc Mwinyi Zahera ameipa umuhimu mkubwa mechi ya ufunguzi ya ligi kuu dhidi ya Ruvu shooting itakayochezwa siku ya jumatano wiki hii huku akiachana na mipango yote ya mechi ya klabu bingwa dhidi ya Zesco united.

”Hatuwezi kuweka akili zetu kwenye mchezo dhidi ya Zesco wakati tuna majukumu ya ligi mbele yetu,tunawaheshimu sana wapinzani wetu kwenye ligi hata michuano ya ligi ya mabingwa kikubwa ni hatua moja kufuata nyingine sasa tunaangalia Ruvu shooting zaidi”.

Aidha timu hiyo imeshindwa kuingia kambini moja kwa moja baada ya kuwapa wachezaji mapumziko ya siku moja ili kupumzisha miili yao kabla ya kuanza maandalizi ya mechi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka