Connect with us

Soka

Wambura Out TPLB

Mtendaji mkuui  wa bodi ya ligi Michael Wambura ameondolewa katika nafasi hiyo baada ya mkataba wake kuisha na shirikisho la soka nchini(Tff) kuamua kutomuongezea mkataba.

Wambura amepewa nafasi ya Mkurugenzi mkuu wa habari na masoko ambayo ni idara mpya ndani ya shirikisho la soka ambapo atakua anasaidiwa na mkuu wa masoko Aron Nyanda na upande wa habari atasaidiwa na Cliffod Mario Ndimbo kwa mujibu wa katibu mkuu wa Tff Alfred Kidao.

Tff imeahidi kuharakisha mchakato wa kumpata mrithi wa wambura ambaye ameliongoza shirikisho hilo kwa miaka minne na kufanikiwa kupandisha thamani ya ligi kuu kutoka shilingi bilioni 3 hadi 6 huku akiongeza idadi ya wadhamini wa ligi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka