Connect with us

Soka

Waliokwama Simba Sasa Freshi

Mastaa wa timu ya Simba sc ambao walikwama kusafiri na timu hiyo kwenda katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Afrika ya kusini kutokana na kutokamilika kwa taratibu za usafiri tayari wamekamilisha na wanatarajiwa kuungana na wenzao muda wowote kuanzia leo.

Mastaa hao akiwemo mfungaji bora wa ligi kuu msimu uliopita Meddie kagere,Deo Kanda,Francis Kahata na kiungo Msudani Sharaff Eldin Shiboub tayari wamekamilisha taratibu hizo ikiwemo masuala ya viza na hati za kusafiria zilizokuwa na matatizo.

Simba imeingia kambini ikiwa na wachezaji wote iliowasajili msimu huu wakiwemo wachezaji watatu raia wa Brazil kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa hivyo kuungana kwa mastaa hao waliokwama nchini itakuwa na furaha kwa kocha Patrick Aussems katika kukiandaa kikosi hicho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka