Connect with us

Soka

Wahispania Wamnyemelea Kagere

Wakati ikidaiwa ameanza kuporomoka kiwango licha kuwa ndio anaongoza katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu,Meddie Kagere amewavutia wahispania ambao wanamuhitaji haraka nchini humo kujiunga na klabu yao.

Timu hiyo ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza  inamuhitaji staa huyo ili kwenda kuongeza nguvu katika harakati za kupanda ligi kuu nchini humo(La liga).

Kagere aliyejinga na Simba sc akitokea nchini Kenya katika klabu ya Gormahia fc ameibuka kuwa mshambuliaji tegemeo klabuni hapo huku akifanikiwa kutwaa tuzo ya mfungaji bora msimu uliopita na tayari ameshafunga mabao 11 msimu akiwa kinara wa ufungaji.

Meneja wa mchezaji huyo Patrick Gakumba tayari amethibitisha kuwasili kwa ofa ya mchezaji huyo huku akisubiria uamuzi wa klabu ya Simba kama itakua tayari kumuuza staa huyo ama kumtoa kwa mkopo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka