Connect with us

Soka

Vodacom Wadhamini Ligi Kuu kwa 9bn

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imeingia mkataba wa miaka mitatu na shirikisho la soka nchini(Tff) kudhamini ligi kuu ya Tanzani bara kwa muda wa miaka mitatu kwa gharama ya shilingi Bilioni 9.

Mkataba huo ulisainiwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Vodacom nchini Hisham Hendi na Rais wa Tff Wallace Karia huku Waziri wa Habari Tamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe akishuhudia utiaji saini huo uliofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo nchini.

Vodacom imerudi kudhamini tena ligi hiyo baada ya kutoongeza mkataba wa awali hali iliyopelekea ligi kuchezwa bila mdhamini mkuu kwa msimu ulioisha lakini baada ya kufikia muafaka huo kampuni hiyo itatoa zawadi zote za washindi katika vipengele mbalimbali katika ligi ya msimu ulioisha ambao mpaka leo zawadi kwa washindi hazijatolewa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka