Connect with us

Soka

Uganda Yapigwa,Yafuzu hatua ya Mtoano

Timu ya taifa ya Uganda imefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon) licha ya jana kufungwa kwa magoli mawili kwa bila na wenyeji Misri waliojipatia magoli hayo kupitia kwa Mohamed Salah kwa mkwaju wa adhabu ndogo na nahodha El-mohammady.

Hata hivyo licha ya matokea hayo timu hizo zote zimefuzu katika hatua inayofuatia ya mtoano ambapo Uganda inaweza kukutana na mshindi kati ya Kenya ama Senegali huku Misri inaweza kukutana na mshindi bora wa tatu katika makundi C,D na E.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo Kongo walifanikiwa kuwafunga Zimbabwe kwa magoli manne kwa bila na kufufua ndoto za kupata nafasi ya kwenda hatua ya mtoano kama mshindi bora wa nafasi ya tatu ambapo nafasi nne zinagombaniwa.

Pia michuano hiyo itaendelea leo ambapo timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) itaikabili Algeria huku Kenya itaikabili Senegal mechi zote zikichezwa saa moja jioni.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka