Connect with us

Soka

Uganda Yaibuka Kidedea Cecafa U20

Timu ya Taifa ya Uganda chini ya miaka 20 imeibuka mabingwa wa michuano ya Cecafa kwa vijana baada ya kuifunga Tanzania mabao 4-1 katika mchezo wa fainali za michuano hiyo iliyomalizika mkoani Arusha.

Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Black Rhino ulishuhudiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia ambaye ni Rais pia wa Cecafa.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Richard Basangwa dakika ya 12, Steven Sserwadda dk 44 ,Ivan Bogere 61  na Kenneth Semakula 72.

Bao la Tanzania lilifungwa na Abdul.H.Suleiman dk 30 kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya Uganda wasepe na taji hilo ambalo lilikuwa mikononi mwa Ngorongoro Heroes.

Cc:SaleheJembe.Blog

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka