Connect with us

Soka

Uganda Wafanya Maajabu Afcon,Zahera Out

Ni kama Timu ya taifa ya Uganda imeshafuzu hatua ya mtoano wa michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri baada ya jana kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Zimbabwe anayoichezea kiungo maarufu wa Yanga Thaban Kamusoko ambaye alicheza mchezo huo japo alitolewa kipindi cha pili.

Emmanuel Okwi anaendelea kuwa shujaa wa Uganda baada kuwafungia goli la kwanza dakika ya 11 ya mchezo akimalizia kazi nzuri iliyoanzia kwa Farouk Miya kisha Khalid Aucho akapiga shuti lililopanguliwa na kipa wa Zimbabwe George Chigova na Mpira kumkuta mfungaji ambaye aliandika goli la kwanza la mchezo na la pili katika michuano hiyo mpaka sasa.

Zimbabwe waliendelea kupambana hasa katikati mwa uwanja na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha baada ya kazi nzuri ya kiungo wa Kaizer chiefs Khama Billiat ambaye alifunga bao la kusawazisha dakika ya 41 na mpaka mchezo unaisha ubao ulisomeka droo na kufanya timu hizo kugawana pointi.

Kwa matokea hayo Misri anaongoza kundi hili la A kwa kuwa na pointi 6 akifuatiwa na Uganda mwenye pointi 4 huku Zimbabwe akishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi moja huku Kongo wakiwa tayari wameshatolewa wakisubiri mchezo wa kukamilisha ratiba baada ya kukubali kichapo cha pili mfululizo dhidi ya Misri na kuifanya timu hiyo inayonolewa na Frolent Ibenge anayesaidiwa na kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kutolewa katika mashindano hayo kinyume na matarajio ya wengi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka