Connect with us

Soka

Tshitshimbi,Gsm Kimeeleweka

Habari za ndani ya klabu ya Yanga zinadai kuwa klabu hiyo imefikia makubaliano ya mkataba wa miaka miwili na nahodha wa klabu hiyo Papy Kabamba Tshitshimbi kuendelea kukichezea klabu hiyo.

Inaelezwa mkataba wa kiungo huyo atavuna mshahara wa shilingi za kitanzania milioni nane huku dau la usajili likidaiwa kuwa ni milioni 100 za kitanzania kwa muda huo wa miaka miwili ambazo zitalipwa kwa awamu.

Mkataba wa Tshitshimbi na klabu hiyo umebakiza miezi minne uweze kufika tamati na tayari alikua akinyemelewa na Simba sc pamoja na Azam Fc huku klabu ya Tp Mazembe nayo ikitajwa kumhitaji kiungo huyo mwenye mapafu ya Mbwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka