Connect with us

Soka

Tff Yatengua Kauli ya Haji Manara

Shirikisho la soka nchini Tanzania(Tff) limeruhusu mashabiki mbalimbali kuingia uwanjani siku ya Jumamosi katika mchezo wa hatua ya mtoano klabu bingwa barani Afrika kati ya Simba sc dhidi ya Plateau United katika uwanja wa Taifa likitengua kauli ya Haji Manara aliyetaka mashabiki wa Simba sc pekee.

Mkuu wa Kitengo cha habari cha Simba sc Haji Manara alitaka mashabiki waliovalia jezi za Simba sc pekee ndio waingie uwanjani kuishangilia timu hiyo katika mchezo huo ambao umeruhusiwa mashabiki elfu 30 pekee.

Tff wamesisitiza katika taarifa yao kupitia mitandao yao ya kijamii kuwa mshabiki yeyote ikiwa havunji sheria anaruhusiwa kuingia uwanja kwani hata timu zenye viwanja hutenga tiketi maalumu kwa mashabiki wa timu pinzani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka