Connect with us

Soka

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano

Kocha wa Manrochester United Ralf Rangnick amemwambia winga Amad Traore kuwa hayupo kwenye mipango yake hivyo wanataka mkumtoa kwa mopo,PSV ya Uholanzi ndiyo inatajwa kuhitaji saini ya kinda huyo.(Manchester Evening News)

Newcastle ina mpango wa kumgeukia mlinzi wa kati wa Sevilla Diego Carlos baada ya mabingwa wa Ufaransa Lille kugoma kumuuza beki wake Sven Botman kwa dau la paundi milioni 30.(Daily)

Nahodha na mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne amekubali kujiunga na Toronto FC inayoshiriki ligi kuu ya Marekani MLS akiwa mchezaji huru pindi mkataba wake na Napoli utakapofikia kikomo mwezi June mwaka huu.(Gazzetta)

Kocha wa Tottenham Antonio Conte amepishana mawazo na mkurugenzi wake wa Ufundi Fabio Paratici kwenye masuala ya usajili.Conte anamtaka kiungo wa Juventus McKenna huku Paratici akimtaka Dejan Kulusevski.(London express)

Mshambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic bado hajatupilia mbali wazo la kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo licha ya kuhitajika na vilabu vya Arsenal,Juventus na Bayern Munich.(skysports Italia)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Joshua Kimmich amerjea kwenye mazoezi ya timu hiyo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Uviko-19 kwa muda wa miezi miwili.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka