Connect with us

Soka

Tetesi za soka Ulaya leo Ijumaa

Liverpool wanavutiwa na mpango wa kumsajili winga wa Arsenal Bukayo Saka ambaye mkataba wake na washika bunduki wa London unamalizika mwaka 2024.(Express)

Liverpool pia wametuma ofa ya mkataba kwa kiungo wa AC Milan Mua Ivory Coast Frank Kessie ambaye mkataba wake na mabingwa mara saba wa kombe la klabu bingwa Ulaya unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Newcastle United wanakaribia kumnasa mlinzi wa kati wa Lill Mdachi Sven Botmann kwa ada ya paundi milioni 30 ikiwa ni usajili wao wa kwanza tangu wachukuliwe na matajiri wa Saudia Arabia.Pia wanataka kumsajili kiungo wa Juventus Aaron Ramsey anayewindwa pia na West Ham.

Wakala wa mshambuliaji wa Manchester Cristiano Ronaldo,Jorge Mendes ametupilia mbali uvumi kuwa mteja wake anataka kuondoka Old Trafford.(skysports)

Arsenal imewaweka kwenye rada mshambuliaji wa Real Sociedad Alexander Isaak na Jonathan David wa Lille ili kuongeza nguvu kwenye idara ya ushambuliaji.(The Athletic)

Mshambuliaji wa Juventus Paul Dybala,beki wa kati Stefan De Vrij na winga Ivan Perisic wa Inter Milan huenda wakashiwishika kujiunga na kocha Antonio Conte Tottenham.(Football London).

Lyon imekataa jaribio la Chelsea kumrudisha kwa mkopo beki wa kushoto Emerson Palmieri baada ya kuumia kwa Ben Chilwel.(L’Equipe).

Newcastle imetenga ofa ya mkataba mnono kwa winga wa FC Barcelona Ousmane Dembele kujiunga na klabi hiyo mwezi Januari.(Foot Mercato)

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka