Connect with us

Soka

Tanzania Yapaa Viwango Fifa

Kufuatia shirikisho la soka duniani(Fifa) kutoa viwango vya mwezi oktoba timu ya taifa ya Tanzania imepanda viwango kwa nafasi mbili zaidi hadi 133 kutoka nafasi ya 135 ya mwezi Septemba.

Kupanda huko kwa Tanzania katika viwango vya soka duniani kunatokana na kufanya vizuri katika baadhi ya michezo ya kimataifa ikiwemo dhidi ya Burundi ambapo licha ya kutoa Sare ugenini ya mabao 1-1 na kufanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa pili hapa Dar es salaam kwa njia ya matuta baada ya sare ya 1-1 dakika tisini za mchezo.

Pia suluhu dhidi ya Rwanda katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Fifa ugenini jijini Kigali pia ni moja ya vitu vilivyochagiza kupanda kwa Tanzania huku pia ikiingia tano bora za ukanda wa soka Afrika Mashariki na kati CECAFA, Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, Sudan, Rwanda na Tanzania.

Kwa Afrika, Tanzania imepanda nafasi 2 juu kutoka 39 hadi 37, Orodha inayoongozwa na Senegal wakifuatiwa na Tunisia, Nigeria, Algeria na Morocco.

Ubelgiji wao ndiyo vinara wa jumla Ulimwenguni, Ufaransa katika nafasi ya pili, Brazil ya tatu, England ya nne na Uruguay nafasi ya tano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka