Connect with us

Soka

Taifa Stars Yalala 1-0

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefungwa bao 1-0 na Tunisia katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon 2021) katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Olympique De Radis mjini Tunis.

Stars iliruhusu bao la penati dakika ya 18 iliyofungwa na Youssef Msakhin kutokana na uzembe wa mabeki kushindwa kujipanga vizuri hali iliyopelekea kipa Aishi Manula kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari.

Kutokana na ushindi huo Tunisia inaongoza msimamo wa kundi J ikiwa na alama 9 huku Tanzania,Libya na Equatorial Guinnea wakiwa na alama 3 kila mmoja huku Stars itarudiana na Tunisia siku ya jumanne Novemba 17 jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka