Ni kama ndio basi tena kwa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) baada ya jana kukubali kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya majirani Harambee stars katika mechi iliyochezwa jijini Cairo katika uwanja wa June 30 nchini humo.
Stars ilianza mchezo kwa presha kubwa na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Saimon Msuva akimalizia shuti lililopanguliwa na kipa Patrick Matasi dakika ya 6′ ya mchezo goli ambalo liliduma mpaka dakika ya 39′ ya mchezo ambapo mshambualiaji anayeichezea timu ya Kashiwa Reyson ya nchini Japan Michael Olunga alipozawazisha kwa tikitaka baada ya kipa Manula kuupangua vibaya mpira ambao ulimgonga beki Erasto nyoni na kisha kumkuta mfungaji.
Harambee stars walitawala eneo la kiungo kutokana na kuwa wachezaji wenye miili mikubwa wakiongozwa na Victor Wanyama anayecheza ligi kuu nchini Uingereza na kuwafanya viungo wa Tanzania Mudathiri Yahaya na Erasto Nyoni kutumia mipira mirefu huku Simon Msuva akifanikiwa kuwasumbua mabeki wa Harambee stars.
Mbwana Samatta aliwanyanyua watanzania baada ya kupachika bao la pili dakika ya 40′ na kuifanya taifa stars kwenda mapumziko kifua mbele.
Dakika ya 62’Johanna Omollo aliisawazishia Kenya kwa kichwa baada ya kuanza kona fupi na baadaye dakika ya 80′ Michael Olunga alizamisha Jahazi la taifa stars kwa goli la tatu kwa shuti la mbali na kuzima ndoto za watanzania kwenda katika hatua ya mtoano.
Msimamo katika kundi hilo la ‘C’ unaonyesha kuwa Algeria tayari ameshakata tiketi ya hatua inayofata huku senegali akiwa katika nafasi ya pili akisubiri mechi ya mwisho dhidi ya kenya ambayo iko nafasi ya tatu na Tanzania ndio imeshika mkia baada ya kupoteza mechi mbili kwa idadi ya magoli matano ya kufungwa na kupoteza matumaini ya kufuzu kama ‘Best looser’.