Connect with us

Soka

Sure Boy Anukia Yanga sc

Baada ya kusimamishwa na klabu yake kwa muda usiojulikana taarifa za ndani kabisa zinasema kiungo Salum Abubakari wa klabu ya Azam Fc anavutiwa na mpango wa kujiunga na klabu ya Yanga sc katika dirisha dogo la usajili linalofunguliwa mwezi january mwakani.

Kiungo huyo kwa muda mrefu amekua akihusishwa kutua Jangwani ikidaiwa mahusiano mazuri baina ya klabu ya Yanga sc na mzazi wa mchezaji huyo yanavutia kiungo huyo kutua Yanga sc.

Sure boy pamoja na wachezaji wenzake Mudathir Yahaya na Aggrey Morris wamefungiwa na klabu ya Azam Fc kwa kinachosemekana kuwa ni utovu wa nidhamu huku ikidaiwa nusu ya wachezaji wa klabu hiyo wana mgomo baridi kushinikiza wachezaji hao warudishwe klabuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka