Connect with us

Soka

Stars,Kenya Hapatoshi Leo Afcon

Hakuna kuangaliana usoni  baina ya nchi jirani za Tanzania na Kenya katika michuano ya Afcon ambapo leo watakutana katika raundi ya pili ya kundi C baada ya timu zote kupoteza kwa kipigo kinachofanana mbele ya Senegal na Algeria.

Mechi hiyo itakayochezwa leo alhamisi saa tano usiku katika uwanja 30 june wenye uwezo wa kuchukua watu elfu 30 waliokaa uliojengwa na jeshi la anga la nchi hiyo na unatumiwa kama uwanja wa nyumbani na timu ya Pyramids fc inayoshiriki ligi kuu nchini Misri.

Mategemeo kwa wakenya yapo kwa staa Victor Wanyama anayeichezea Tottenham ya ligi kuu Uingereza huku kwa upande wa Tanzania matumaini yakibebwa na Mbwana Samata mfungaji bora wa pili ligi kuu nchini Ubeligiji akiichezea Krc Genk ya nchini humo.

Eneo la ushambuliaji la Harambee stars litakaloongozwa na Michael Olunga anayeichezea kashiwa Reyson ya Japan linatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka kwa mabeki wa taifa stars wakiongozwa na Kelvin Yondani huku pia kurejea kwa majeruhi Erasto Nyoni kumeleta nafuu kwa stars.

Mshindi katika mechi hiyo atakuwa amejiweka nafasi nzuri ya kupata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano huku akiombea mechi kati ya Algeria na Senegal mmoja apoteze ili kuleta nafuu kwa timu hizo za Afrika mashariki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka