Connect with us

Soka

Stars Yamtibulia Kibarua Migne

Shirikisho la soka la Kenya (FKF) limesitisha ajira ya kocha wa timu hiyo mfaransa Sebastien Migne kutokana na matokeo yasiyoridhisha ya timu ya taifa (Harambee stars) katika michuano mbalimbali hivi karibuni.

Harambee stars licha ya kufanya vibaya katika michuano ya Afcon nchini Misri pia hivi karibuni ilitolewa na Taifa stars katika michezo ya awali kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa raundi ya pili jijini Nairobi.

Katika taarifa iliyotolewa na shirikisho la nchini humo ilisomeka “Shirikisho la soka la Kenya na kocha Sebastien Migne tumekubaliana kusitisha mkataba baina yetu,hata hivyo shirikisho linamshukuru Migne kwa kufanikiwa kuwezesha kufuzu michuano ya Afcon baada ya miaka 15”.

Migne ataungana na orodha ndefu ya makocha waliotimuliwa baada ya kufanya vibaya katika michuano ya Afcon akiwemo kocha wa Taifa stars Emmanuel Amunike.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka