Connect with us

Soka

Stars Hali Tete

Timu ya taifa ya Tanzania(taifa stars) ipo katika hatihati ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) baada ya jana kukubali kipigo cha bao moja kwa bila kutoka kwa Sudan katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa.

Stars ilihitaji ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ugenini katika mchezo wa marudiano lakini uzembe wa mabeki kushindwa kuokoa krosi iliyochongwa kutoka upande wa kulia ulisababisha goli hilo lililofungwa na Yasir Mzamil dakika ya 60.

Stars itabidi ijilaumu yenyewe baada ya kukosa nafasi za wazi kupitia kwa Ayoub Lyanga,Gadiel Michael,Miraj Athuman na Shaban Idd chilunda huku kipa Juma Kaseja akionyesha ubora wake golini.

Stars italazimika kushinda mchezo huo ili kujikatia tiketi ya kwenda Cameroon katika michuano hiyo.Katika mchezo huo stars iliwakilishwa na : Juma Kaseja, Boniface Maganga, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Salum Abubakar, Shaban Chilunda, Ayubu Lyanga, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude na Idd Seleman.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka