Connect with us

Soka

Spurs yapigwa chini na UEFA

Shirikisho la soka barani uUlaya(UEFA ) limeiondosha klabu ya Tottenham Hotspurs katika michuano ya Uefa conference league baada ya kushindwa kufanyika kwa mchezo wake wa mwisho dhidi ya Rennes ya Ufaransa.

Mchezo huo uliopangwa kufanyika Diesemba 9 mwaka huu haukufanyika baada ya Tottenham kuripoti idadi kubwa ya maambuzikizi ya Uviko -19 kutoka kwa wafanyakazi na wachezaji wake,hali iliyopelekea kuahirishwa kwa mchezo huo.

Lakini baada ya kikao cha ndai UEFA imeamua kuipa Rennes ushindi wa mabao 3-0 pamoja na alama zote tatu za mchezo huo uliokuwa unaamua hatima ya timu ipi ingefuzu hatua ya mtoano kati ya timu hizo.

Kutokana na maamuzi hayo Rennes ya Ufaransa imemaliza nafasi ya kwanza huku Vitesse ya Uholanzi ikimaliza nafasi ya pili na kufuzu hatua inayofuata.

Taarifa huenda ikawa ni nzuri kwa kocha wa kikosi hicho Antonio Conte ambaye atapata muda wa kutosha kuiandaa timu kwaajili ya michezo ya ligi kuu ambayo wana nafasi kubwa ya kufuzu michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao endapo watapata matokeo mazuri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka