Connect with us

Soka

Sportpesa Yawatega Simba,Yanga sc

Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa Sportpesa Tanzania  Abbas Tarimba amesema mwaka huu (2020) hakutakuwa na Mashindano ya Sportpesa kutokana na kuyumba kwa uchumi wa kampuni hiyo kulikotokana na mlipuko wa Corona.

Pia Mkurugenzi huyo amebainisha hawana uhakika kama wataongeza mikataba mipya ya udhamini katika klabu za Simba sc, Yanga sc na Namungo sababu ikiwa ni kuyumba kwa uchumi kwa kampuni hiyo sababu ya Corona.

Ikumbukwe nchini Kenya kampuni hiyo ilijitoa kudhamini baadhi ya klabu ikiwemo klabu bingwa mara (19) ya ligi ya Kenya Gormahia na kusababisha kuyumba vibaya kwa uchumi wa vilabu hivyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka