Connect with us

Soka

Sofapaka yamtimua Mreno

Klabu ya Sofapaka FC ya Kenya imetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo raia wa Ureno, Divaldo Alves kufatia matokeo ya kusua sua inayoyapata klabu hiyo.

Kocha huyo ameshinda michezo miwili huku akitoa sare miwili na kufungwa minne katika ya michezo nane hali  ambayo haikuwafurahisha mabingwa hao wa ligi kuu mwaka 2008.
Kocha huyo alitimuliwa siku ya jana wakati akijiandaa na mechi ya ligi kuu nchini kenya dhidi ya Wazito fc huku taarifa ya klabu hiyo ikieleza kuwa wamemtimua kutokana na matokeo mabovu.
“Tumeachana na kocha Alves kutokana na matokeo mabovu,amewasilisha barua ya kuacha kazi na tumeikubali” alisema bosi wa timu hiyo.
Hata hivyo timu hiyo imemteua John Baraza kuwa kocha wa timu hiyo kushika nafasi ya mreno huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka