Connect with us

Soka

“Sina Mkataba Yanga”-Morrison

Bernard Morrison afunguka juu ya mkataba wake katika klabu ya Yanga sc baada ya taarifa kusambaa kuwa alisaini mkataba mpya wa miaka miwili kabla ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha.

Kiungo huyo kutoka Ghana anayekipiga ndani ya Yanga SC amesema mkataba wake wa sasa unaisha mwezi ujao (July 2020) na hajasaini mkataba mpya kama ilivyoripotiwa na uongozi wa klabu huku pia akibainisha kwamba mechi mbili za awali alicheza bila kuwa na mkataba.

Pia staa huyo raia wa Ghana amekwenda mbali zaidi na kusema hafurahishwi na mwenendo wa uongozi wa Jangwani na mpaka sasa anakipiga kwasababu ya heshima kubwa anayoipata kutoka kwa mashabiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka