Connect with us

Soka

Simba,Yanga zaanza vema Mapinduzi

Klabu za Simba na Yanga zimezanza vizuri mechi zao za kwanza za kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi wa 2-0 kila moja na kuweka mzaingira mzauri ya kufuzu hatua ya nusu fainali a michuano hiyo.

Simba waliokuwa wa kwanza kucheza majira ya saa kumi jioni ilifunga Selem view ya Pemba 2-0 kwa mabao ya mchezaji aliye kwenye kiwango bora kwasasa Pape Sakho dakika ya 25 kabla ya Rally Bwalya kuongeza la pili dakika ya 53.Katika mchezo huo kiungo Bwalya aliibuka mchezaji bora na kujipatia zawadi ya Tsh 500,000 kutoka kwa waandaaji.

Yanga walicheza majira ya saa mbili usiku na kujipatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Taifa Jang’ombe kwa mabao safi kutoka kwa Mkongomani Heritier Makambo dakika ya 31 na usajili mpya Denis Nkane dakika ya 49.

Wachezaji walio kwenye majaribio ndani ya Simba Shiboub na Moukoro walipata dakika za kuonesha kila walichonacho huku Denis Nkane na Crispin Ngushi nao wakicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Yanga baada ya kusajiliwa hivi karibuni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka