Connect with us

Soka

Simba Yaua Mtu Bondeni

Leo asubuhi Simba sc ilikua na mechi ya kirafiki na timu ya Orbret Tvet ya nchini humo katika kujiandaa na msimu wa ligi kuu na michuano ya kimataifa ambapo timu hiyo imeibuka na ushindi wa magoli 4-0.

Katika mchezo huo uliokua na mapumziko kila baada ya dakika 30 Simba ilipata magoli kupitia kwa  nahodha John Boko aliyefunga mabao mawili na Hassan Dilunga akifunga moja huku Mbrazili Wilker Da silva nae akifunga goli moja.

Katika mchezo huo simba ilionyesha soka safi licha ya kupata ushindi huo mnono na inatarajiwa kucheza mchezo mwingine siku ya kesho dhidi ya Platnum stars.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka