Connect with us

Soka

Simba Yahamia 5G

Baada ya kufungwa mchezo wa mwisho na Mbao fc,Klabu ya Simba sc imerejesha furaha kwa mashabiki baada ya kuifunga klabu ya Alliance fc mabao 5-1.

Katika mchezo huo mabao ya Simba sc yalipatikana kupitia Meddie Kagere  dakika ya 24 kwa penalti bao ambalo lilisawazishwa na Martin Kigi wa Alliance dakika ya 38.

Dakika ya 44 Kagere alitupia bao la pili na kumfanya afikishe jumla ya mabao 22 kwa sasa huku Luis Miqquisone akifunga la tatu dakika ya 63 na dakika ya 66 Deo Kanda alifunga bao la nne huku Said Ndemla akifunga bao la mwisho dakika ya 87.

Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 84 kibindoni huku Alliance ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 41 zote zimecheza jumla ya mechi 36.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka