Connect with us

Soka

Simba Wachezea Kichapo

Timu ya Simba imepoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc uliomalizika jioni hii kwa goli 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kambarage jijini Shinyanga.

Mwadui ilipata bao pekee la mchezo huo dakika ya 32 ya mchezo likifungwa kwa kichwa baada ya kupokea krosi kutoka upande wa kushoto na kumkuta mfungaji Gerrad Mathias aliyekua amekabwa na mabeki wawili wa Simba lakini alipiga kichwa kilichomshinda kipa Aishi Manula.

Simba imebakiwa na pointi 18 ikicheza michezo saba ya ligi kuu huku ikiendelea kubaki kileleni licha ya kupoteza mchezo huo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka