Connect with us

Soka

Simba Sc Wapangwa na Wanigeria

Klabu ya Simba sc imepangwa na timu ya Plateau United FC Kutoka Nchini Nigeria Katika Raundi ya Awali ya Msimu wa Klabu Bingwa Afrika 2020/21.

Katika droo hiyo iliyochezeshwa jana nan shirikisho la soka barani Afrika(Caf) inaonyesha kuwa timu hizo zitakutana nchini Nigeria katika mchezo wa utangulizi kati ya tarehe 27–29 Novemba 2020 na Marudiano ni Kati ya tarehe 4–6 Desemba 2020 Kwa Mujibu wa ratiba ya awali Kama hakutakuwa na Mabadiliko mengine.

Plateau wamekuwa Wawakilishi wa Nigeria Baada ya Kuwa vinara wa ligi kuu nchini humo Wakati Msimu wa ligi unafutwa sababu ya Janga la Corona – Mshindi wa jumla wa mtanange huu, atacheza na Mshindi mwingine wa jumla Kati ya Costa do Sol Kutoka Msumbiji au FC Platinum ya Zimbabwe.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka