Connect with us

Soka

Simba Sc Vs APR Hakuna Mbabe

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na alama tatu katika mchezo wa kundi B michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 katika dakika tisini za mchezo huo uliokua mkali na wa kusisimua huku ukijaza mashabiki wengi katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar.

Ikianza na kikosi chenye mastaa wengi wa kikosi cha kwanza ambapo golini alisimama Hussein Abel huku Israel Mwenda na Duchu wakicheza pembeni na walinzi wa kati wakiwa ni Kennedy Juma na Hussein Kazi na eneo la kiungo akisimama Fabrice Ngoma na Sadio Kanoute huku Shabani Idd Chilunda,Saido Ntibanzokiza,Jimson Mwinuke na Michael Charamba wakianza kama washambulizi.

Simba sc pamoja na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga bado ilizidiwa eneo la katikati na viungo wa Apr ambao walionyesha soka safi huku wakishambulia kwa mipango huku mpaka dakika tisini zinamalizika mashabiki walipata burudani ya kutosha.

Kutokana na matokeo hayo Simba sc na Apr zote zimefuzu hatua ya robo fainali ambapo zitaungana na Singida Fountain Gate kucheza hatua ya robo fainali itakayoanza siku ya Jumapili huku Apr itakutana na Yanga sc Simba sc dhidi ya Jamhuri huku Singida Fountain Gate itakutana na Azam Fc na Jamus dhidi ya KVZ.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka