Connect with us

Soka

Simba sc na usajili wa kimya kimya

Mabingwa watetezi wa soka nchini Simba sc wanajiandaa kuisimamisha nchi katika siku hizi nne zilizobaki kuelekea kufungwa kwa dirisha dogo la usajili linalotarajia kufungwa Januari 15 siku ya Jumamosi majira ya saa 5:59 usiku.

Katika michuano ya Mapinduzi inayoendelea huko visiwani Zanzibar timu hiyo imeleta wachezaji wa Kimataifa kwaajili ya majaribio na kama atapatikana atakayefanya vizuri basi atasajiliwa,wachezaji hao ni Shiboub,Tenena na Udor.Lakini kwa kinachoendela haioneshi kama yupo atkayesalia nchini kati ya hao.

Mchezaji wa kiungo cha chini Udor ameonekana kuwakosha wengi kutokana na uwezo wake katika eneo hilo hasa katika upigaji wa pasi,changamoto kubwa kwake ni ubora wa wachezaji wanaocheza katika nafasi yake ambao ni Jonas Mkude na Tadeo Lwanga,lakini ukomo wa idadi ya wachezaji wa kigeni huenda ikazua kusajiliwa kwake.

Hilo linatokana na klabu hiyo kuwa kwenye hatua za mwisho kumtangaza mchezaji wao wa zamani Clatous Chama anayerudi nchini kwa mara nyingine baada ya kuchemka katika klabu ya RS Berkane ya Morocco.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka