Connect with us

Soka

Simba mbabe mbele ya Azam

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba sc imeendelea rekodi nzuri ya ushindi dhidi ya waoka mikate Azam fc pindi timu hizo zinapokutana.

Katika mchezo uliofanyika Jumamosi hii na kupewa jina la ‘Derby ya Mzizima’ Mnyama ameibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kupunguza gepu la alama na wapinzani wake wa jadi Yanga waliocheza siku ya Ijumaa na kupakia kuwa ni pointi tano huku Simba akiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mechi hiyo kali kabisa iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa ilishuhudia timu hizo zikienda mapumziko bila kufungana,kipindi cha pili Simba walianza kwa kuwashambulia sana Azam hadi kufanikiwa kufunga bao dakika ya 67 kupitia kwa Sadio Kanoute.

Dakika ya 71 kiungo mshambuliaji kutoka Senegal Pape Ousmane Sakho aliwaandikia Simba goli la pili akimalizia vizuri pasi ya Kibu Denis,Rodgers Kola aliifunga azam goli la kufutia machozi dakika ya 79.

Timu hiyo sasa wamefikisha alama 24 kati ya michezo 10 iliyocheza hadi kufikia sasa,na wanajiandaa kuelekea Zanzibar kushiriki kombe la Mapinduzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka