Connect with us

Soka

Simba Kumenoga,Mo Atema Cheche

Tajiri wa klabu ya Simba Mohamed Dewji ametoa zawadi za pikipiki,simu za mkononi na rice koka kwa kila mchezaji wa timu hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa timu hiyo endapo itachukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Mo aliahidi zawadi ya pikipiki kwa kila mchezaji endapo watatwaa taji hilo lakini ameongeza simu za mkononi na kifaa cha kupikia wali kwa umeme(rice cooker) baada ya timu hiyo kufuzu robo fainali ya michuano ya klabu bingwa afrika kwa msimu ulioisha.

Zawadi hizo zimetolewa na mwakilishi wa makampuni ya mfanyabiashara huyo Fateema Dewji ambapo Simba iliwakilishwa na mtendaji mkuu Senzo Masingiza na kocha Patrick Aussems pamoja na nahodha John Boko huku baadhi ya wachezaji wakihudhuria tukio hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka