Connect with us

Soka

Simba Hoi Kwa Wamakonde

Timu ya Simba sc imetolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kukubali kutoa sare ya 1-1 na timu ya Ud Songo kutoka Msumbuji katika mchezo wa marudiano uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam baada ya ule wa awali kutoka suluhu nchini Msumbiji.

Ud Songo waliwaduwaza mashabiki waliojaa uwanja wa taifa baada ya kucheza soka la kushambulia na kufanikiwa kupata goli la kwanza kwa njia ya faulo dakika ya 16 lililofungwa na Luis Misquissone na kuwafanya wenyeji kutawala mchezo mpaka mapumziko licha kukosa nafasi nyingi za wazi.

Kipindi cha pili Simba ilikuja na kasi ya kushambulia lakini kukosekana kwa mshambuliaji John Boko ilionesha kuwaangusha wenyeji licha ya krosi nyingi zilizopigwa na Deo Kanda na pasi mpenyezo za Cletous Chama kukosa mmaliziaji baada ya Meddie Kagere kuwa chini ya uangalizi mkali.

Simba walifanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 87 kwa njia ya penati na kujitahidi kuongeza goli la pili lakini hadi mpira unaisha matokea yalibaki sare hivyo mabingwa hao wa ligi kuu mara mbili mfululizo kutolewa kwa bao la ugenini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka