Connect with us

Soka

Simba Bado Tatu Ubingwa

Klabu ya Simba sc imebakiza pointi 3 kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Mbeya city mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mabao mawili ya Nahodha John Boko dakika ya 5 na 74 yalitosha kuihakikishia klabu hiyo pointi tatu muhimu mbele ya kocha wa Mbeya city Amri Said ambaye ameichezea klabu Simba sc kwa mafanikio miaka ya nyuma.

Simba sc inahitaji kushinda mchezo ujao dhidi ya Prisons ili kujihakikishia Ubingwa wa ligi kuu baada ya kufikisha pointi 81.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka