Connect with us

Soka

“Simba Bado Sana”-Aussems

Aliyekuwa kocha wa Simba sc Mbeligiji Patrick Aussems amesema kuwa timu hiyo bado haijawa tayari kupambana katika michuano ya kimataifa licha ya kufanya vizuri katika ligi ya ndani.

Aussems aliyeifikisha timu hiyo hatua ya robo fainali kabla ya kutolewa na Tp Mazembe alisema bado timu hiyo kiuchezaji haijaiva .

” Malengo yao najua  ni kuona wanafanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao na hilo lipo mikononi mwao kwani wanaongoza ligi wakiwaacha wapinzani wao lakini kufikia hatua ya robo fainali itakuwa ngumu.

“Ninajua  haliwezi kutokea kwa sababu siasa za viongozi na kila mmoja atahitaji kuona cha kwake ndiyo sahihi na ugumu wa michuano kimataifa kwa timu zenye malengo upo wazi ila siyo Simba,” amesema.

Simba kwa sasa ndio wanaongoza ligi kuu nchini na wanaelekea kutangazwa kuwa mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo endapo watashinda nusu ya mechi zilizosalia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka