Connect with us

Soka

Serikali Yapiga Stop Mashabiki Viwanjani

Serikali imepiga marufuku mashabiki wa soka katika mikoa nje ya Dar es Salaam, kuingia viwanjani kutazama mechi za Ligi Kuu zitakazohusisha timu za Simba na Yanga kuanzia leo (Jana) hadi pale itakapojiridhisha .

Agizo hilo limetolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kufuatia kukiukwa kwa miongozo iliyowekwa ya kukabiliana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika juzi katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, baina ya Mbeya City na Simba .

Katika taarifa yake iliyotolewa jana jioni, serikali imesema imechukua hatua hiyo baada ya kubaini kutofuatwa kwa miongozo iliyowekwa na serikali kwa ajili ya kukabiliana na virusi hivyo .

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka