Connect with us

Soka

Senzo Akabidhiwa Mabadiliko Yanga

Mchakato wa mabadiliko katika klabu ya Yanga sc imefikia hatua nzuri baada ya rasimu yenye mabadiliko kutoka La liga kukabidhiwa kwa mshauri mkuu wa klabu hiyo Senzo Mazingiza tukio lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Rasmi hiyo yenye kurasa mia nne itachambuliwa kitaalamu na kamati ya mabadiliko ya klabu hiyo chini ya wakili Dk.Alex Mgongolwa kabla ya kuletwa kwa wanachama kwa ajili ya mapitio na kufanya uamuzi kupitia  mkutano mkuu wa klabu hiyo.

Meneja wa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga SC, Eng. Hersi Said amesema gharama zote za mchakato wa mabadiliko, zinalipwa kwa asilimia 100 na Wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM.

“Leo Yanga tunaandika historia kwa kuleta mfumo wa uendeshaji wa klabu yetu kutoka kwenye Dunia ya kwanza kwenye soka kwa maana ya La liga ya Hispania”

“Mfumo huu unakwenda kuirudisha klabu kwa wanachama na wao ndio watakuwa wamiliki halali wa klabu na baada ya mfumo kukamilika, niwahakikishie tu watu wote sio tu Tanzania bali Afrika nzima watakuja kwetu kujifunza,”Alisema Eng.Hersi Said

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka