Connect with us

Soka

Samatta “Out” Uefa

Timu ya Krc Genk anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta imetolewa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 mbele ya Napoli katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa San Paulo jijini Napoli.

Mabao ya Napoli yalipatikana dakika za 2,26 na 78 kupitia kwa Arkadiusz Milk aliyefunga hat trick huku bao la nne likipatikana kwa njia ya penati mpigaji akiwa ni Dries Mertens.

Kwa matokeo ya jana ya kundi hilo la E  Liverpool na Napoli wanafuzu hatua ya 16 bora huku Genk na Redbull Salzburg wakiyaaga mashindano japo Salzburg ataingia hatua ya pili ya ligi ya Europa.

Genk wameyaaga mashindano hayo wakiwa hawajashinda hata mchezo mmoja huku Samatta akiweka rekodi ya kufunga mabao matatu katika michuano hiyo mikubwa barani ulaya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka