Connect with us

Soka

Samatta Amfuata Mo Salah

Mshambuliaji wa KRC Genk na Timu Ya Taifa Ya Tanzania Mbwana Samatta amebadili kampuni ya uwakala aliyokuwa nayo mwanzo ya First For Players na kujiunga na Spocs Consultant kwa ajili ya kumsimamia Katika maswala ya mikataba, uhamisho, na usajili.

Spocs Consultant ndiyo kampuni inayomsimamia Mohamed Salah wa Liverpool katika maswala yote ya uhamisho, Samatta, aliingia mkataba na First For Players December 22 2018 .

Kampuni hiyo ni kubwa katika biashara ya michezo duniani ikijihusisha na michezo kwa ujumla wake ikiwemo kusimamia wachezaji,kutafuta vipaji,kutengeneza biashara huku wakifanya kazi kwa ukaribu na vilabu na mashirikisho ya soka duniani.

Baadhi ya wachezaji waliochini ya kampuni hiyo ni kama ifuatavyo:

  • Abdul Rahman Baba
  • Mohamed Salah
  • Mohamed Elneny
  • Ahmet Hamoudi
  • Andreas Ivanschitz
  • Marc Janko
  • Ivan Ivanov
  • Isaac Vorsah
  • John Duku Antwi
  • Abdalla Gomaa
  • Benjamin Tetteh
  • Emmanuel Adjei Sowah
  • Stanley Ohawuchi
  • Mahmoud Hassan (Trezeguet)
  • Omar Gaber
  • Mohammed Dauda

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka