Connect with us

Soka

Samata Bado Yupo Epl

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amefanikiwa kusalia ligi kuu ya Uingereza baada ya timu yake ya Aston Villa kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Westham United.

Endapo Aston Villa ingepoteza mchezo moja kwa moja ingeshuka daraja lakini bao la Jacky Grealish dakika ya 84 ambalo lilisawazishwa na Andriy Yarmolenko lilitosha kuwabakisha huku Watford wakifungwa na Arsenal na kuwarahisishia kazi.

Timu Zilizoshuka daraja ni pamoja na Bournemouth iliyo nafasi ya 18 na pointi 34, Watford iliyo nafasi ya 19 na pointi 34 na Norwich City iliyo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 21.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka