Connect with us

Soka

Salamba Atua Namungo Fc

Mshambuliaji wa zamani wa Lipuli Fc Adam Salamba amesajiliwa na timu ya Namungo Fc kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Simba sc baada ya kutopata nafasi kikosi cha kwanza katika timu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye mwili wa soka aliibukia katika klabu ya stand united na kupata umaarufu wakati akiichezea Lipuli fc chini ya kocha Selemani Matola na baada ya msimu mmoja alisajiliwa na wanamsimbazi lakini changamoto ya namba mbele ya wakongwe Meddie Kagere na John Boko imemuondoa kikosini.

Namungo iliyopanda daraja msimu huu imefanikiwa kusajili wachezaji kadhaa wakiwemo kutoka nje ya nchi ili kuimarisha kikosi hicho chenye makazi yake Ruangwa mkoani Mtwara ikitumia uwanja wa Majaliwa kama uwanja wa nyumbani.

Salamba amelazimika kujiunga na timu hiyo baada ya jitihada ya kucheza nje ya nchi hasa Afrika ya Kusini kugonga mwamba licha ya kufanya majaribio mara kadhaa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka