Connect with us

Soka

Salamba Aibukia Uarabuni

Mshambuliaji wa Simba sc Adam Salamba amejiunga na timu ya Al Jahra sc inayoshirikiligi kuu nchini Kuwait kwa dau linalokadiriwa kufikia shilingi milioni 100.

Salamba aliyesajiliwa na Simba sc akitokea Lipuli Fc alishindwa kupata nafasi kikosini hapo mbele ya Meddie Kagere na John Boko hali iliyosababisha atolewe kwa mkopo kwenda Namungo baada ya dili lake kujiunga na timu moja kutoka Afrika kusini kushindikana.

Al jahra ilianzishwa mwaka 1966 na inapatikana katika mji wa Jahra nchini kuwaiti ikiwa imeshriki ligi kuu nchini humo mara 21 na ikiwa inamiliki uwanja wa nyumbani wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 17000.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka